Mwanadada Maarufu mtandaoni Esma Platnumz ambaye pia ni dada wa msanii Diamond Platnumz amefunguka na kusema kuwa clip ya sauti inayosambaa kwenye mitandao sio ya kwake.
Clip hio ya sauti ambapo mtu anayesadikika kuwa ni Esma Platnumz anasikika akiongea na simu kuelezea jinsi gani alivyoingiliwa na mwanaume kinyume cha maumbile imesambaa sana baada ya kupostiwa na mwanadada maarufu kwa habari za Umbea Mange Kimambi.
Esma amekanusha vikali kuwa sio yeye katika mahojiano yake na kipindi cha mashasham cha wasafi Fm huku akisema kuwa imemwingiza katika mgogoro na mpenzi wake na kusisitiza kuwa watu wote wanaomjua wanajua yeye hana tabia kama ambazo zinazungumziwa kwenye clip hyo.
“Mimi mwenyewe nashangaa,Boyfriend wangu ndo alikuwa wa kwanza kunitumia,baadae simu zikawa nyingi kuwa kuna mtu amepost sauti na kusema kuwa ni mimi. Yeye kama ameamua kunichafua mimi nalipokea lakini yule sio mimi..Boyfriend wangu ,marafiki zangu hata ex wangu ananifahamu vizuri mimi sio wa hivyo” Alifunguka Esma.