HABARI

Mwijaku : Nandy Lazima Anilipe Hela Yangu,Nitamwinda Mpaka kaburini.

 

Sakata la kuvuja kwa sauti za Nandy linaendelea kuchukua sura mpya,hii ni baada ya Mwijaku ambaye anashtumiwa kuvujisha sauti hizo kudai kuwa atafanya lolote ili kuhakikisha kuwa Nandy anamlipa hela yake.

Mwijaku ambaye licha ya kukataa kuwa yeye ndiye amevujisha sauti zile amekiri kuwa zile ni sauti za Nandy na alikuwa anazungumza na yeye na ni kweli kwamba walikuwa na dili ambalo mpaka leo Nandy hajamlipa hela yake.

“Mimi ni mtu wa marketing ,nmemsadia ku edit proposal na kumuunganisha kwa mdhamini inabidi nilipwe,na tulikubaliana kiasi kikubwa zaidi baada ya kukamilisha dili ila kwa kumwonea huruma kutokana na mihangahiko ya harusi nikapunguza kiwango”,alifunguka Mwijaku akiwa kwenye kipindi cha Super Breakfast cha Clouds FM

Hata Hivyo Mwijaku ameonekana kuwa amedhamiria kushika mashati na Nandy mpaka amlipe hela yake hiyo.

About the author

kidevu

Leave a Comment