HABARI

Dudu Baya awachana Baba Levo na Sallam Sk,waache kuropoka.

 

Msanii mkongwe wa Muziki WA bongo fleva Dudu baya amenijitokeza hadharani na kuwachana Baba Levo pamoja na Sallam Sk kwa kitendo cha kumshambulia mtayarishaji nguli wa kizazi kipya ,P Funk Majani.


Dudu Baya amedai kuwa kwa heshima na mambo makubwa ambayo Majani amefanya kwenye tasnia hii wawili hao hawakupaswa kumshambulia kiasi cha kumuhusisha na maswala yake binafsi yanayomhusu P funk,mzazi mwenzake Kajala na Paula.

Dudu Baya amedai kuwa ukiachana na biashara kila mtu ana mambo take binafsi hata yeye baba Levo mbona ameachana na mama WA motto wake na ameolewa pengine,na kuongeza kuwa hata Sallam ameshatarikiana mara nne.

Dudu Baya alisema hayo baada ya kuona kuwa Baba Levo na Sallam wanamshambulia Majani kuwa ameibiwa mke na Harmonize na pia motto wake wa kike anatembea na Rayvan.

About the author

kidevu

Leave a Comment