Mwimbaji na mtangazaji maarufu kutoka Kenya Tanasha Donna amefunguka na kusema kuwa hatamani mwanae arithi kazi wanayoifanya wazazi wake yani kuwa msanii.
Tanasha ambaye pia ni mzazi mwenza wa mwanamuziki maarufu kutoka Tanzania Diamond Platnumz amefunguka hayo kwenye mahojiano yake ya hivi karibuni na kusema kuwa muziki unakuja na siasa nyingi amabazo ni chafu na kudai kuwa anatamani mwanae awe mwanamichezo.
“Nadhani inawezekana ,kwa sababu baba na mama yake wote ni wasanii ila Mungu Ndiye anajua.Ila kwa upande wangu ningetamani awe mwanasoka kwa sababu najua watu wa kwenye soka wana nidhamu ya hali ya juu,kwa sababu kwenye muziki kuna siasa nyingi ambazo watu hawazijui japo akiamua kuwa mwanamuziki nitamsapoti pia”.alisema Tanasha.