HABARI

Shabiki Afunguka Alivyofungwa Jela Kisa Harmonize.

 


Katika hali isiyo ya kawaida kijana APhiz Phino ,mchoraji ,mkazi wa kigoma ambaye amedai kuwa yeye ni shabiki namba moja wa Harmonize amefunguka namna ambavyo mapenzi yake kwa msanii huyo yalimsbabishia matatizo kiasi cha kuwekwa kizuizini kwa muda wa wiki moja.

Kijana hiyo anadai kuwa alichora picha ya harmonize na lengo lake lilikuwa ni kumkabidhi msanii huyo alipokuja kutumbuiza kwenye kampeni za urais ,lakini kutokana na taratibu kuwa ngumu za kumfikia ilibidi avunje utaratibu na kwenda kupanda jukwaani wakati Harmonize anatumbuiza lakini kwa sababu ya ulinzi mkali maaskari waliweza kumdhibiti na kumweka kizuizini ambapo alikaa ndani kwa takribani siku 8 kabla ya kuachiwa.


This time around shabiki huyo amepata nafasi ya kuonana na Harmonize na kumpatia zawadi ya picha kubwa aliyoichora kwa ajili yake ,yote hayo yametendeka siku ya jana ambapo Harmonize alitua kwa ajili ya onesho lake.

About the author

kidevu

Leave a Comment