Kwa Mara ya kwanza Diamond Platnumz amefunguka kuhusu shtuma zinazomkabili yeye na lebo take ya wasafi kwamba wanawanyonya wasanii kwa kuwapa mikataba mibovu.
Katika mahojiano yake na kituo cha DW akiwa nchini Ujerumani Diamond Platnumz amekanusha tuhuma hizo na kusema kuwa kama Lebo yake ingekuwa inawanyonya wasaniii wake basi wasingekuwa na hela kiasi cha kujiita matajiri huku akitamba kuwa ukitoa yeye kwa hapa Tanzania wasanii wa WCB ndio wanaoongoza kuwa na pesa nyingi.
Diamond ameweka wazi kuwa mara nyingi wasanii wanahisi kuwa wananyonywa kwa sababu wanaona pesa zinazoingia ni nyingi zaidi tofauti na wanazopewa lakini wanasahau kuwa mgawo ni mkubwa pia na Lebo inataka irudishe uwekezaji wake.
“Sisi tunachofanya ni biashara,tunawachukua vijana kutoka chini kabisa na kuwafanya kile wachofanya kiwe kikubwa,Sasa inapokuja biashara kuwa kubwa wengi wa Vijana wanataka ile biashara aichukue peke yake,yani ile fedha aikusanye peke yake wakati ni investment iliwekwa.Kwa hiyo ikifika hapo mtu anataka aondoke tu,unasepa vipi wakati hii ni biashara..yani niwekeze milioni zaidi ya 500 kwenye muziki wako halafu hela zikianza kuingia unataka ukimbie haiwezekani” alifunguka Diamond Platnumz.