HABARI

Diamond Platnumz na Zuchu Sio Siri Tena,Wajiachia Paris Bila Woga

 

Baada ya kuwepo tetesi kwa muda mrefu kuwa boss wa WCB Diamond Platnumz yuko kwenye dimbwi zito la mahaba na mwimbaji wa kike kutoka kwenye lebo hiyo Zuchu,wawili hao wameamua kutoka katika kifungo cha kujificha na kuweka mambo hadharani.


Ni muda mrefu sasa toka iripotiwe kuwa wawili hao wako kwenye huba zito japo wao wenyewe hawakutaka kuweka dhahiri kuwa wanatoka kimapenzi zaidi ya kuonyesha viashiria vichache ambaye mtu yoyote mwenye akili angejua ukweli huo.

Inaonekana wazi kuwa uzalendo umemshinda Diamond na kuamua kuyaanika mahaba aliyonayo juu ya msanii huyo namba moja kwa upande wa wanawake ,ambapo Diamond amepost videos akijiachia na kula bata na mpenzi wake huyo wakiwa jijini Paris Ufaransa.

Ni kama vile Diamond ameamua kujipa likizo baada ya kazi nzito ya kufanya ziara ya EP yake huko Ulaya na akaona sio vyema kuruka peke yake hivyo akaamua kumvuta mpenzi wake huyo ambaye katika video ameonyesha wakiwa wanalandalanda sehemu za bata .Hapo chini ni baadhi ya picha kutoka kwenye video ambazo Diamond alipost.

About the author

kidevu

Leave a Comment