Kwa mara ya kwanza toka atoke chini ya Usimamizi wa Konde Music Worldwide msanii wa rap Country boy amefunguka kuhusu mwelekeo wake wa kimuziki akiwa chini ya kampuni yake mpya IAM MUSIC.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari Country pia aliweka wazi kuwa amelamba dili la ubalozi kutoka moja ya saloon hapa mjini lakini pia yuko mbioni kuachia kazi zake na za vijana wake ambao amewa sign kwenye lebo yake.
Alipoulizwa na waandishi kuhusu uhusiano wake na aliyekuwa boss wake Harmonize,Country alidai kuwa yeye hana tatizo lolote na msanii huyo ambaye alimsaini kwenye lebo ya Konde Music Worldwide lakini pia aliweka wazi kuwa hawako karibu kwa sababu ya ufinyu wa mawasiliano baina yao akimaanisha kuwa huwa hawapigiani simu.
Alipoulizwa kuhusu Diamond Platnumz,Country Boy aliweka wazi kuwa Diamond ni mtu ambaye anapenda kazi zake na wamekuwa wakipanga mara nyingi wafanye kazi ila ratiba zao zimekuwa ngumu na kuweka wazi kuwa msanii ambaye yuko naye karibu zaidi ni Rayvan ambaye huwa wanakutana mara kwa mara hata kuwasiliana kwenye simu.