KLABU ya Al Ahly ya Misri baada ya kupoteza mchezo wa leo Februari 23 kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Simba Uwanja wa Mkapa wameanza safari ya Kurejea Misri.
Simba imeshinda bao dakika ya 30 kupitia kwa Luis Miquissone ambalo lilidumu mpaka dakika ya 90, Uwanja wa Mkapa.
Hivyo baada ya kuyeyusha pointi tatu mbele ya Simba ambao ni vinara katika kundi A wameamua kurejea nchini Misri kwa ajili ya mipango mingine.
Kocha wa Al Ahly, Waarabu wa Misri, Pitso Mosimane amesema kuwa anaamini vijana wake kuna kitu wamejifunza na wataendelea kupambana kufikia malengo yao.
Simba inakuwa imeshinda mechi mbili mfululizo kwenye mchezo za Ligi ya Mabingwa Afrika, mchezo wa Kwanza walishinda ugenini bao 1-0 dhidi ya AS Vita na leo bao 1-0 dhidi ya Al Ahly.