HABARI

NADO: AZAM FC TUTAFANYA VIZURI NDANI YA LIGI, MASHABIKI WATUPE SAPOTI

 


 WINGA wa Azam FC,  Idd Seleman, ‘Naldo’ amesema kuwa wana imani ya kufanya vizuri ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21.


Nyota huyo amekuwa kwenye ubora ndani ya Azam FC ambayo inanolewa na Kocha Mkuu,  George Lwandamina akisaidiana na Vivier Bahati ambaye ni msaidizi wa kikosi hicho. 


Azam FC imetupia jumla ya mabao 29 baada ya kucheza mechi 21 yeye ametupia jumla ya mabao sita na mara ya mwisho kufunga ilikuwa Uwanja wa Azam Complex kwenye sare ya ushindi wa  mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City.


Kinara wa Ligi Kuu Bara ni Yanga akiwa amekusanya jumla ya pointi 49 baada ya kucheza mechi 21 anafuatiwa na Simba mwenye pointi 42 na amecheza jumla ya mechi 18.


Nado amesema:”Kazi bado inaendelea na kila mchezaji anatambua kwamba ushindani ni mkubwa hivyo tutazidi kupambana ili kupata matokeo mazuri katika mechi zetu zijazo.


“Bado kuna mechi nyingi za kucheza na kila timu ina nafasi ya kufanya vizuri, mashabiki waendelee kutupa sapoti kila kitu kitakuwa sawa,”.

Azam FC msimu huu wa 2020/21 imesepa na pointi zote sita mbele ya mabosi wa zamani wa Nado, Mbeya City, kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza Uwanja wa Sokoine walishinda bao 1-0 na ule wa pili Uwanja wa Azam Complex, Azam FC ilishinda mabao 2-1.

About the author

kidevu

Leave a Comment