HABARI

KMC YAANZA MAANDALIZI FA NA LIGI KUU BARA

 

UONGOZI wa KMC umeweka wazi kuwa kwa sasa umeanza maandalizi kwa ajili ya mechi zao za Kombe la Shirikisho pamoja na Ligi Kuu Bara.

Mchezo wake wa mwisho wa ligi KMC iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kagera Sugar, mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru.

Kwa sasa imeanza maandalizi kuelekea kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Kurugenzi FC unaotarajiwa kuchezwa Ijumaa, Uwanja wa Uhuru.

Baada ya kumalizana na Kurugenzi itakuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Polisi Tanzania na Coastal Union ya Tanga.


Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwangala amesema:”Februari 26 tutakuwa na mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Kurugenzi FC,hatujawahi kucheza nao ila tunaamini kwamba tutapambana kupata matokeo. 


“Mechi zetu mbili za ligi itakuwa ugenini mbele ya Polisi Tanzania na Coastal Union, tupo tayari na tunahitaji pointi tatu muhimu ndani ya uwanja,”.

About the author

kidevu

Leave a Comment