Kwenye mitandao ya kijamii wiki iliyopita kuhusiana na kumsema Mwana Fa, msanii Q Chief ameeleza kuwa neno lake ni dawa ndiyo maana bado ana umuhimu hadi leo watu wanamzungumzia kuhusu video ile.
Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii, Q Chief ameonekana kwenye video fupi akimsema Mwana Fa kwamba ametafuta kiki na amefanya kitendo cha kitoto kwa kujitangaza kama amepata virusi vya ugonjwa wa Corona jambo ambalo lilimfanya kumuongelea vibaya.
Akizungumzia kuhusu kutrend kwa video hiyo mitandaoni na kumsema Mwana Fa amesema,
“Kila mtu na dunia nzima inamjua Q Chief sio lazima ufe ndiyo watu ndiyo wakusifie na kauli yangu ni kama dawa, mimi sio mtu wakushinda mitandaoni kila muda, video ile kutembea kiasi hicho inamaanisha bado nina umuhimu kwa watu na wanaamini kile ninachokisema”.
Pia ameongeza kusema “Kuna muda haitakiwi watu wote wa kuamini au kuwa na imani na wewe, lakini unaweza ukatoa mawazo ambayo itawanyima watu wengine raha au usingizi”