Mdau anasema kwa kipindi kirefu kumekuwa na uwekezaji wa miundombinu ya barabara kuu na za vitongoji ambazo zinajengwa kwa kiwango cha lami ila kwa bahati mbaya lami hii huwa haidumu hata kidogo
Anadai, maeneo mengi watumishi wa barabara wanakumbwa na adha ya mashimo (potholes) karibuni kila kona, ambayo hukua na kugeuka kuwa mashimo makubwa sana na huwa ni hatarishi kwa usalama wa raia na vyombo vyao
Anahoji kwanini Serikali isijifunze kwa Mataifa makubwa ambako barabara zao kubwa kuliko za kwetu zimejengwa kwa kiwango cha zege na zinadaiwa hudumu kwa muda mrefu kuliko barabara ya Lami
Maoni yako ni yapi kuhusu hoja hii?