HABARI

Hatimae Benitez na kikosi chake Dalian Yifang warejea China

Hatimae kocha Rafael Benitez na kikosi cha timu yake Dalian Yifang wamerejea China baada ya kukaa kwa muda mrefu nchini Hispania sababu za mlipuko wa virusi vya corona nchini China.
Dalian Yifang ni club ya China na inafundishwa na kocha Rafael Benitez hivyo walikuwa camp nchini Hispania kwa ajili ya maandalizi ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu ya China na walilazimika kuendelea kukaa Hispania.
Dalian Yifang wanarejea China baada ya China maambukizi kudhibitiwa huku Ulaya ikionekana kuwa virusi hivyo ndio vimeshika kasi kwa kuenea, wachezaji wa Dalian na staff wao baada ya kurejea China watakaa Quarantine kwa siku 14 na watafanya hivyo wakiwa katik kambi y uwanja wao wa mazoezi.

About the author

kidevu

Leave a Comment