Wakati Mataifa mbalimbali yakisimamisha shughuli za michezo ambayo ni chanzo moja wapo cha mkusanyiko wa watu, huku Uefa ikifikiria namna ya kuweka sawa ratiba za msimu lakini nchi hiyo kwao soka lilikuwa likipigwa bila hofu.
Wakati Uturuki Super Ligi ikiwa ya mwisho kusimamisha michezo yake siku ya Alhamisi, taifa hilo la Belarus linalopatikana Mashariki mwa Ulaya bado ligi inaendelea kuchezwa.
“Dunia nzima sasa inaangalia Belarusian league. Kila mtu anakwenda kwenye luninga yake kutuangalia sisi.” Amsema Hleb
Alexander Hleb ameongeza “Wakati NHL ilipofunga msimu, wachezaji wengi wa ‘ice hockey’ walikwenda Urusi kucheza. Pengine Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wanaweza kuja Belarus league kuendelea kucheza huwezi juwa.”
“Ni semehu pekee barani Ulaya unaweza kucheza mpira wa miguu, wala mamlaka hazijawa tayari kusimamisha michezo.”
Wakati Mataifa ya Ulaya yakizidi kuchukua tahadhari dhidi ya Corona, Rais wa Belarus, Alexander Lukashenko kwa upande wake amependeka matrekta ‘tractor therapy’ kutumika viwanjani kama sehemu ya kupambana na virusi vya corona