Rais wa Marekani Donald Trump amekuwa akitetea kuhusu jinsi alivyokabiliana na mlipuko wa virusi vya corona nchini Marekani.
Hatu ayake ya hivi punde ni ya kuzuia safari za ndege kutoka Ulaya kuingia nchini Marekani.
BBC imechunguza madai ya Trump kuhusu mlipuko wa virusi vya corona nchini mwake. Je anasema Ukweli?
“Marekani imefanya kazi nzuri ya kupima, wakati watu wanahitaji kupimwa.“
Mapema mwezi Machi , Ikulu ya Marekani ilisema kuwa Marekani hawana vifaa vya kutosha vya kujikinga .
Baadhi ya vituo vya afya pia viliripotiwa kupata wakati mgumu wa kutumia vifaa hivyo.
Serikali inasema kuwa watu zaidi ya milioni moja wamepewa vifaa hivyo, huku vingine vikitarajiwa kuwasili katika maeneo husika.
Vifaa vya kupima virusi vya corona kutoka kituo cha kudhibiti na kuzia magonjwa
Lakini Marekani imewapima watu wachache zaidi ya nchi nyingine- watu milioni 26 kati ya Januari, 3 na Machi, 3 ukilinganisha Korea kusini ambapo walipima watu 4,000.
Uingereza ilifanya vipimo vipimo 400 kwa watu milioni na Italia 1,000 mnamo 10 Machi.
Wataalamu wa afya wana hofu kuwa virusi vimeenea Marekani bila kujulikana kwa sababu ni watu wachache walipimwa.
Madai ya pili
Rais Trump alisema mwezi Machi 11 : “Tumeokoa maisha kwa kuchukua hatua haraka dhidi ya China. Na sasa lazima lazima tuchukue tahadhali ile ile kwa Ulaya.”
Rais Trump mara nyingi amenukuliwa akitaja marufuku ya usafiri kwa sababu idadi ya visa vya corona nchini Marekani iko chini na maisha ya wengi yameweza kuokolewa.
Januari 31, taifa lolote geni ambalo lilikuwa China ndani ya siku 14 zilizopita walikuwa wanakatazwa kuingia Marekani.
Ndege tatu kubwa nchini Marekani zilizokuwa zinafanya safari zake China zilisitisha safari zake.
Baadae mwezi Februari, katazo liliwekwa kwa wageni wanaotokea Iran – ambao tayari walikuwa katika marufuku ya usafiri .
Raia ambao si Marekani kutoka nchi 26 za ulaya walipigwa marufuku kuingia Marekani.
Raia wa Marekani na familia zao hawakuhusishwa na marufuku zote.
Wataalamu wanaamini kuwa hatua ya Marekani ilipaswa kuwapa muda serikali kujiandaa na kupunguza idadi ya visa vya corona lakini hatuna uhakika kuwa inasaidia kulinda maisha ya watu.
Shirika la afya duniani (WHO) ilisema kuwa kuweka zuio la watu kusafiri ni hatari zaidi, kwa sababu kwa kufanya hivyo kutaweka wakati mgumu kwa mzunguko wa upatikanaji wa madawa na kuathiri uchumi.
Madai ya tatu
Ukiulizia kuhusu takwimu za WHO kuhusu virusi vya corona, Rais Trump alisema Machi 5,: “Nadhani 3.4% si idadi sahihi…Binafsi , idadi iko chini hata ya 1%.”
Katika mahojiano ya simu katika Fox News, rais Trump alisema kuwa takwimu za WHO za 3.4% kuhusu virusi vifo vya corona sio vya kweli .
WHO imeripoti kuwa Machi 3, takwimu zote ziligusia visa vyote vya vifo vya corona.
Bwana Trump alisema kwamba alidhani kuwa takwimu za vifo ni sahihi.
Alisema kuwa idadi ya vifo imeonekana kuwa kubwa kwa sababu watu wengi walipata maambukizi ya mwanzo ya virusi hivyo bila ya kwenda kupata matibabu.
Kuna uhaba wa takwimu za walioathirika na kufa na ugonjwa wa corona.
Madai ya nne
Mwezi Machi ,9 alisema: “Mwaka jana Wamarekani 37,000 walikufa kutokana na mafua.Hakuna kilichofungwa, maisha na uchumi uliendelea... Embu fikiria hilo.”
Wakati huuu rais alieleza kwa hafahamu ni wamarekani wangapi walihusishwa na mafua hayo. .
Lakini kituo cha kuthibiti magonjwa (CDC) kilitoa takwimu ya kati ya vifo 26,339 na 52,664 vilivyotokana na mafua wakati wa baridi na kukiwa na makadirio kuwa kati ya mwezi oktoba mpaka Febrari 2020, watu 34,157 watakuwa wamekufa.
Hivyo ni watu wengi wanakufa na mafua kila mwaka, bwana Trump aliainisha hilo.
Ingawa virusi vipya vya corona havina chanjo wala dawa, Ingawa wanasayansi wanaamini kuwa idadi ya vifo vya mafua wakati wa baridi iko juu zaidi.
Madai ya tano
Bwana Trump alisema kuwa Machi, 7 : “Hivi punde tutakuja na chanjo.”
Kwa sasa hakuna chanjo ya virusi vipywa vya corona, ingawa nchi nyingi wanafanya jitihada zote za kupata kinga hiyo.
Wanasaysansi wanasema kuwa labda mpaka katikati ya mwaka kesho.
Majaribio ya chanjo kwa wanyama tayari yameanza na kama majaribio kwa wanadamu yataanza baadae mwaka huu pia.
Madai ya sita
Februari 26, rais alisema: “Tumechukua hatua zote kali ambazo hazijafanywa na mataifa mengine ili tujikinge maambukizi ya virusi vya corona.“
Kama tunavyofahamu kuwa Mareani iliweka marufuku ya usafiri na kuweka watu karantini lakini Marekani wanashauriwa kuwa hatua kali walizoweka dhidi ya corona si jambo sahihi.
China na Italia, kwa mfano, wameweka wigo mkubwa wa kuweka watu karantini kwa sababu ya mamilioni ya watu walioathirika.
Marekani inapaswa kuiga kutoka kwao au kufanya jambo ambalo linafanana na hilo.