HABARI

Waziri athibitishwa kupata Corona Iran

                                          

Naibu Waziri wa Afya wa nchi ya Iran, Iraj Haririch amegundulika kupatwa na maambukizi ya Virusi vya 2019-nCoV ambavyo husababisha ugonjwa hatari wa Corona ambao tayari watu zaidi ya 80,000 wameripotiwa kuambikizwa na wengine zaidi ya 2,765 wakifariki kutokana na ugonjwa huo.
Mapema jana jumanne kupitia akaunti yake ya mtandao wa tweeter, Waziri huyo wa Afya amesema “naomba niwaambie kuwa nimepata maambukizi ya Corona”.
Waziri huyo alionyesha dalili za ugonjwa huo ikiwemo homa kali na baada ya kupimwa akaonekana ana maambukizi ya ugonjwa huo ambao tayari umeripotiwa kuua watu 16 na kuambukiza zaidi ya watu 95 nchini  Iran.
Waziri huyo ametengwa katika hospitali maalumu akipatiwa matibabu na amethibitisha kuwa anaendelea vizuri baada ya kupata matibabu.

About the author

kidevu

Leave a Comment