HABARI

Imam Bahloul: Mwanamke aliyefufua mjadala wa wanawake kuongoza ibada misikitini

                               Imam Bahloul
                                                       Imam Bahloul mwenye miziz ya Ufaransa na Algeria

Jina la msomi wa masuala ya Kiislamu Imam Bahloul lilirejelewa mara kwa mara Ijumaa iliopita baada ya swala ya Ijumaa tarehe 21 mwezi Februari na waumini walikuwa wanaume kwa wanawake waliokusanyika katika ukumbi mmoja mjini Paris.
Hatua hiyo iliochukuliwa na Kaheneh sio ya kwanza, kwani baadhi ya wanawake wameitekelza katika mataifa ya Marekani na barani Ulaya.
Tangu kukamilika kwa mwaka 2018, Kahaneh raia wa Ufaransa kutoka kwa baba wa Algeria, amepata umaarufu sana katika vyombo vya habari, na ameonekana katika zaidi ya runinga moja baada ya kumpatia mwalimu wa filisofia na mwandishi Faker Korshan pendekezo la kuanzisha msikiti kwa jina Fatima Mosque mjini Paris.
Lakini msikiti huo hautakuwa ukifuata tamaduni iliopo.
Kundi moja la imamu huyo limeanza kukusanya mchango wa kujenga msikiti mjini Paris utakaojumuisha wanawake na wanaume chini ya paa moja na wanawake wasio na hijabu wataruhusiwa kuchaganyika na wanaume na wanawake wenzao wanaovaa hijab katika msikiti huo.Profesa wa sayansi ya siasa kutoka Swiss Ilham Manea aliongoza ibada katika msikiti wa Berlin
           Profesa wa sayansi ya siasa kutoka Swiss Ilham Manea aliongoza ibada katika msikiti wa Berlin

Maombi yatafanyika kwa kuongozwa na wanaume na mara nyengine wanawake kila baada ya wiki moja na huo utakuwa msikiti wa aina yake kuwahi kuwepo nchini Ufaransa.
Kuhusu lengo la mradi huu, Imamu huyo wa kike aliambia BBC Arabic mnamo mwezi Julai mwaka jana kwamba anadhania kwamba mwanamke huyo mwenye umri mdogo atawaruhusu vijana Waislamu kuuangalia Uislamu kwa jicho tofauti .
”Vijana wengi wanawaona wanaume misikitini kama wanaume, wanaume wazee. Maono yao kuhusu Uislamu ni ya zamani na sio ya kisasa”.Inada ya siku ya ijumaa katika ukumbi mmoja wa Paris tarehe 21 mwezi februari
Tayari ametanya mchanganyiko itafanyika kwasababu za kiusalama.
Lakini Imamu huyo hataki mradi wake kuanza mara moja, baada ya kundi lake kukodisha ukumbi mmoja mjini Paris kwa ibada za siku ya Ijumaa ambapo alitoa hotuba kuhusu upendo wa Mungu na baadaye akangoza maombi.
Miaka 15 iliopita 2005 Amina Wadudu, profesa wa masomo ya Kiislamu katika chuo kikuu cha Virginia nchini Marekani, aliongoza ibada ya Ijumaa iliokuwa na mchanganyiko wa wanaume na wanawake , na ilisemekana kwamba hiyo ililkuwa hatua ya kwanza kwa mwanamke kuongoza ibada ya mchanganyiko wa wanaume na wanawake.
Misikiti kadhaa ilikataa kuandaa ibada hiyo na waandalizi wake walificha kutaja eneo ambapo ibada hiyo ilitarajiwa kufanyika kwa muda kutokana na vitisho , na iliamuliwa ibada hiyo kufanyika katika kanisa moja la Kianglikana mjini New York.Amina Wadud
                                      Profesa wa chuo kikuu cha England Oxford
Misikiti mitatu mjini New York ilikataa kufanya ibada na imamu huyo na ukumbi mmoja wa Sanaa ulipokea vitisho vya kulipuliwa iwapo utaruhusu ibada kama hiyo kufanyika ndani yake.
Kama imamu wa Bahloul , Amina Wadud alitoa hotuba ya Ijumaa kabla ya ibada ambayo iliandaliwa na kundi moja la wanaharakati na waandishi na mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu na lengo lake ilikuwa kufunguwa majadiliano ya kuhusu utenganishaji wa wanaume na wanawke wakati wa ibada na kuruhusu maimamu wanaume pekee kuongoza ibada.
Jina la Amina kabla ya kubadilika kuwa Muislamu alikuwa Mary Teasley.
Suala la uongozi wa wanawake limesalia kuwa tata na kukataliwa na wengi duniani. Muhubiri wa Kiislamu Yusuf al- Qaradawi alitaja kile ambacho Amina Wadud alikifanya kuwa ‘uvumbuzi mbaya’ katika chuo kikuu cha Sheikh Al- Azahar mjini Cairo ambapo alisema kwamba Uislamu hauruhusu wanawake kuwahubiria wanaume.
”Ni makosa kwa wanaume kuangalia miili ya wanawake iliopo mbele yao”, alisema Sheikh al Azhar, Sayed katika gazeti la Misri Al- Ahram.Profesa wa chuo kikuu cha Oxford mjini England Amina Wadud
                                             Amina wadudu akiongeza ibada ya siku ya Ijumaa 2008

Kila mwanamke alikataa kuwaongoza wanawake kwasababu kadhaa. Kwa mfano , Muhubiri Yasmine Mujahid, mwandishi wa Marekani na muhadhiri aliandika katika facebook kuhusu wadhfa wake kuhusu uongozi wa wanawake.
“Wanawake wa Magharibi wanalazimika kudhibitisha thamani ya mwanamke kwa kumlinganisha na mwanaume”
Mwanamume akikata nywele zake pia mwanamke anafaa kukata nyewle zake, Akijiunga na jeshi pia yeye anataka kujiunga na jeshi na mengine mengi.

About the author

kidevu

Leave a Comment