HABARI

Coronavirus: Uhaba wa kemikali za kunawa mikono washuhudiwa Kenya

A security guard gives hand disinfectant to visitors as precaution measures at an entrance of building in Nairobi, Kenya - 13 March 2020

Hali ya wasiwasi yatanda nchini Kenya baada ya kisa cha kwanza cha virusi vya Corona kuthibitishwa kupitia Wizara ya afya.
Ijumaa, waziri wa Afya bwana Mutahi Kagwe alisema kwamba mtu mwenye maambukizi ya virusi vya Corona alithibitishwa kuwa na maambukizi hayo Alhamisi usiku.
Baada ya tangazo hilo, raia walionekana wakikimbilia kwenye maduka ya jumla kununua kemikali za kuua viini vya bakteria mikononi maarufu kwa kiingereza kama ”hand sanitisers” pamoja na barakoa za kufunika uso.
Wateja walioanza kumiminika nyakati za mchana walikuwa na wakati mgumu kupata bidhaa hizo zilizokuwa adimu ghafla za kemikali za kunawa mikono zinazoua viini mara moja na barakoa.
Mteja mmoja aliyetembelea duka la jumla alihakiishiwa kwamba bidhaa hizo zitapatikana asubuhi ya leo kwa sababu zimeagiza kwa wingi lakini pia akaombwa kufika mapema kwasababu ni bidhaa zinazokimbiliwa na wengi.
Baadhi ya wateja walilazimika kununua bidhaa zingine mbadala za kuua viini mfano wa zile zinazotumika wakati wa kuosha nguo mara nyingi ikiwa ni zile za watoto wadogo, lakini wakati huu zikilengwa kumimininwa kwa kaisi kidogo katika maji ya kunawa mikono au kuosha sakafu.
Licha ya kwamba, maduka ya jumla na yale ya kuuza dawa yameahidi upatikanaji wa bidhaa hiyo kwa kiwango kikubwa, baadhi ya wateja wanahofia kwamba huenda bei za bidhaa hizo ikapanda maradufu kwasababu ya uhitaji wake wakati huu.An empty hand sanitiser shelf in Superdrug in London
      Uhaba wa bidhaa za kemikali za kuosha mikono zinazoua viini washuhudiwa nchini Kenya huku mgonjwa wa kwanza wa Corona akithibitishwa

Serikali ya kenya imefahamisha raia kwamba hakuna haja ya kuwa na hofu licha ya kuthibitishwa kwa kisa cha kwanza cha mgonjwa wa Corona.
Kulingana na mwandishi wa BBC kitengo cha Afya Rhoda Odhiambo, katika mitandao ya kijamii kuna mengi ambayo yanapotosha kuhusu ugonjwa wa Corona.
Kwa sasa ni kwamba hakuna haja ya kununua kwa wingi kemikali za kuosha mikono zinazoua viini kwa haraka au hata kununua bidhaa kwa wingi kwasababu ya hofu ya ugonjwa huu.
Mwandishi wa BBC Anne Ngugi alitembelea katikati mwa mji mkuu jijini Kenya ambapo biashara zilikuwa zinaendelea kama kawaida.
Kulingana na raia mmoja aliyekutana naye ambaye tayari alikuwa amevalia barakoa, Gilbert Bairon, amepatwa na mshtuko mkubwa kwa sababu ni jambo ambalo hakulitarajia na kutoa wito kwa Wakenya wajihadhari kwasababu kulingana na yeye huu ni ugonjwa unaosambaa tena kwa haraka.
Mama mmoja ambaye hakujitambulisha amesema kwamba hadi wakati huo hakuwa amejipanga kwa lolote kwasababu ndio alikuwa tu amepata habari.
Alipoulizwa ikawa yupo tayari kufunga biashara yake iwapo hatua kama hiyo itafikiwa alisema kwamba kwa sasa cha msingi ni kumuomba tu Mungu isifikie hatua hiyo kwasababu hajui atakachofanya.
Mfanyabiashara mmoja wa bodaboda aliyejitambulisha kama Ruto, alisema kwamba anachojiuliza ni iwapo serikali itafikiria kuwaletea kinga kwasababu kazi kama yake ni kubeba wateja ambao hawajui na mara nyingi humkaribia.
Wasiwasi mkubwa wa mfanyabishara Ruto ni kwamba huenda akambeba mteja mwenye virusi vya Corona bila kujua na akamuathiri.Wataalam wa afya ya umma wamekuwa wakitoa ushauri ili kujaribu kuzuia maambukizi ya virusi hivi.
Wataalam wa afya ya umma wamekuwa wakitoa ushauri ili kujaribu kuzuia maambukizi ya virusi hivi
1. Kunawa mikono mara kwa mara.
2. Kutokaribiana sana na mtu mwingine ambaye anakohoa ama kupiga chafya – simama umbali wa mita moja
3. Watu wanaokohoa ama kupiga chafya wasalie majumbani mwao ama kutojichanganya na makundi ya watu
4.Hakikisha kwamba unaziba pua na mdomo unapokohoa kwa kutumia kitambaa ama tishu.
5. Mtu anayehisi joto ama tatizo la kupumua ametakiwa kusalia nyumbani.
6. Tumepiga marufuku mikutano ya aina yote ikiwemo ile ya umma kama vile ya kidini, michezo, na wanaotaka kwenda makanisani na msikitini watalazimika kuosha mikono na sabuni kabla ya kuingia katika sehemu hizo.
7. Michezo yote inayohusisha shule imepigwa marufuku lakini shule zote zitasalia wazi kwa wakati huu.
8. Wachukuzi wa umma wametakiwa kuhakikisha kuwa abiria wanaosha mikono yao kabla ya kuingia katika magari hayo.
9. Amewaonya Wakenya kutosambaza habari za uongo kuhusu virusi hivyo katika mitandao ya kijamii ambazo zinaweza kusababisha hofu.
10. Wakenya wamewekewa zuio la kutoka nje ya nchi isipokuwa wale wenye umuhimu mkubwa wa kusafiri na hakuna mtu atakayeruhusiwa kuelekea katika mataifa yenye visa vingi vya ugonjwa huo.
11. Serikali imesema kwamba itatoa maelezo kuhusu ugonjwa huo kila siku.
Waziri huyo amesema kwamba Kenya inaelekea katika wakati ambapo sekta za kibinafsi na zile za kibiashara zitalazimika kuisaidia serikali na raia katika kuchukua jukumu la kukabialana na janga hili.

About the author

kidevu

Leave a Comment