HABARI

Mmiliki wa Olympiacos na Nottingham Forest apona corona

Mmiliki wa club ya Nottingham Forest na Olympiacos Evangelos Marikanis ,52, aliyetangaza kuwa na maambukizi ya virusi vya corona siku kadhaa nyuma.
Evangelos Marikanis alitangaza kuwa na maambukizi na baada ya kukaa karantini kwa siku 14 (wiki mbili) amethibitisha kuwa amepona virusi hivyo na yupo sawa kuendelea na mfumo wa maisha yake ya kawaida.
Bilionea Marikanis anamiliki miradi mbalimbali kama timu ya Olympiacos ya nchini kwao Ugiriki na Nottingham Forest ya England lakini pia ni mmiliki wa meli kadhaa, utajiri wake ni dola milioni 650 za kimarekani (Tsh Trilion 1.4).

About the author

kidevu

Leave a Comment