Muigizaji Idris Elba ameibuka na kujibu wanaosema kuwa Mastaa wanalipwa kujitangaza wamepata virusi vya Corona, Tetesi ambazo zilianzishwa na rapper Cardi B siku chache zilizopita.
Kupitia InstaLive nyota huyo wa filamu ya ‘Hobbs & Show’ alifunguka kuwa tetesi hizo hazina maana yoyote “Wazo hili kwamba mtu kama mimi naweza kulipwa kusema nina ugonjwa, Ni jambo ambalo halina maana, Huu ni Ujinga na watu wanataka kueneza utadhani kama ni habari. Huu ni ujinga … na njia ya haraka ya kuwafanya watu wapate maambukizi”
Siku chache zilizopita #CardiB bila kutaja jina la staa yoyote alihoji kuhusu mastaa wanaojitangaza kupata corona kuwa wote wanadai hawana dalili zozote sasa ilikuwaje wakaenda kupima?