HABARI

WHO: Marekani huenda ikawa kitovu kipya cha COVID-19

Shirika la Afya Ulimwenguni – WHO limesema kuwa Marekani huenda ikawa kitovu kipya cha ulimwengu cha mlipuko wa virusi vya corona baada ya idadi ya visa vya ugonjwa huo kupanda kwa kasi nchini humo.
Image result for WHO Margaret Harris us may be became
Msemaji wa WHO Margaret Harris amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva kuwa katika kipindi cha saa 24 zilizopita, asilimia 85 ya visa vipya vimetokea Ulaya na Marekani.
Image result for WHO Margaret Harris
Msemaji wa WHO Margaret Harris
Kati ya visa hivyo, asilimia 40 ni vya kutokea Marekani. Kimataifa, idadi ya visa vilivyothibitishwa vya virusi vya corona imepindukia 337,000 kote katika nchi 194 kufikia leo asubuhi, kwa mujibu wa takwimu za shirika la habari la Reuters, huku kukiwa na zaidi ya vifo 16,500 vinavyo husishwa na virusi hivyo.
Kwa mujibu wa chombo cha habari cha DW, Nchi ya China imetangaza leo kuondoa vikwazo vya usafiri katika eneo ambalo lilikuwa kitovu cha janga la virusi hivyo, wakati serikali kote duniani zikiimarisha hatua za kuwazuia watu kusafiri.

About the author

kidevu

Leave a Comment