HABARI

TANZIA: Nguli wa muziki wa Afro Jazz Manu Dibango kutoka Cameroon, Afariki kwa virusi vya Corona akiwa Ufaransa

Mwanamuziki, mwandishi na mpuliza saxophone maarufu Duniani EMANUEL N’DJOKE DIBANGO ( MANU DIBANGO) mzaliwa wa Cameroon amefariki Dunia kwa Ugonjwa wa Virusi vya Corona leo.
Kutoka katika ukurasa wake wa Facebook taarifa za kifo chake ziliandikwa
“Ni machungu na huzuni kubwa kutangaza kwamba DIBANGO amefariki leo 24 -3-2020 akiwa na umri wa miaka 86”. Moja kati ya visa vya kukumbukwa ni pale marehemu Manu Dibango alipodai hakimiliki kutoka kwa gwiji wa Pop duniani Michael Jackson kwa kutumia vionjo vya SOUL MAKOSSA ya Dibango katika wimbo wa Wanna Be Startin’ Somethin’ wa Michael Jackson.
Dibango alitamba sana katika upulizaji saxophone, muziki wa Jazz, uandishi wa nyimbo na hata kuchanganya vionjo vya asili toka Cameroon na kuvipaza katika majukwaa ya kimataifa Duniani. Dibango ameacha watoto watatu, Georgia Dibango, Marva Dibango, Michael Dibango. Mungu ailaze mahala pema peponi roho ya marehemu DIBANGO.

About the author

kidevu

Leave a Comment