HABARI

Baba mwenye nyumba asamehe kodi ya miezi miwili kisa corona

Baba mwenye nyumba mmoja amewaachia Wapangaji wake tabasamu la nguvu kwa kuwafutia kodi ya nyumba ya miezi miwili ili watumie hizo pesa kujiandaa dhidi ya corona lakini pia kuwapa nafuu kipindi hiki ambacho kazi na biashara hazifanyiki kutokana na kuepuka kusambaa kwa corona.
Baba mwenye nyumba huyo wa Nyandarua Kenya amesema “tunajua corona itaathiri Watu wote wakiwemo Wafanyakazi ambao wengine wao wanaoishi kwenye nyumba zangu, inatupasa tushirikiane Serikali na Wananchi na tusaidiane wenyewe kwa wenyewe”.
Mpaka March 25 2020 Kenya ilikua na Wagonjwa 25 wenye virusi vya corona huku Mgonjwa wa kwanza kukutwa na virusi hivyo tayari amepona ambapo Serikali ya Nchi hiyo imeendeleza mapambano dhidi ya kirusi corona, tayari Rais Kenyatta ametangaza kupunguza mshahara wake kwa asilimia 80 na Mawaziri 30% ili pesa hizo zikasaidie mapambano hayo.

About the author

kidevu

Leave a Comment