SAKINA LYOKA AKIWA NA MUMEWE ABDILLAH WAKIFURAHIA TUKIO HILO ADHIMU. |
Mtangazaji wa clouds televisheni kipindi cha ng’aring’ari Sakina lyoka amezungumza na mtandao huu na kusema kwamba anafurahia mno ndoa yake na mumewe Abdillah kwani naamini kwa sasa nimepata nilichokuwa nakitafuta kwa muda mrefu nasema ahsante mungu kwa kunipatia mume mwema.
Kuolewa sio ajabu ila kikubwa ni pale unapojaaliwa kumpata alie mwema katika ndoa yako nikimaanisha mume! alisema Sakina huku akimlalia mumewe miguuni kwa raha zao!, nae Abdillah kwa upande wake alisema Sakina ni mwanamke wa maisha yangu nilipiga goti kwa mungu aweze kunipa mke bora ambae tutaenda katika maisha na kweli amenipa Sakina wangu nampenda sana na naahidi kumtunza na nitamlinda kwa kila khali alisema Abdillah.
SAKINA LYOKA AKIMSHUKURU MUNGU KWA NDOA YAKE KUTIMIA. |
Ndoa hii ambayo ilifungwa mwezi wa kumi na mbali mwaka jana na kumaliziwa na shetehe kubwa katika ukumbi uliopo mbezi, mtandao huu uliamua kumtembelea sakina LYOKA nyumbani kwako na kutaka kujua ni kwa kiasi gani anaona ndoa yake hiyo mpya tokea aolewe na huu utakuwa ndio utaratibu wa mtandao huu kutembelea ndoa za mastaa wetu ili kumfahamu je kunani?. Sisi tunampongeza Sakina pamoja na mumewe kwa maelewano mazuri na tunawatakia mafanikio makubwa katika ndoa yao.