HABARI

KHADIJA KOPA ASEMA, KAPTEN TEMBA HANIDAI CHOCHOTE…SINA DENI NAE!.

Malkia wa mipasho nchini tanzania khadija omary kopa jana jumapili akiwa ndani ya east africa redio na bibie Mwanne Othman mtangazaji wa kipindi cha taarab amejibu kiaina  shutuma zilizozagaa mitandaoni kwamba anadaiwa shilingi laki tatu za kitanzania na mtunzi wa mashairi Kapten temba mchaga wa kwanza kuimba taarab nchini.


Mkongwe huyo wa taarab nchini alisema kwamba sipendi kumzungumzia huyo mtu sababu naona kama nampa kiki kutajwa na mtu maarufu kama mimi ila naomba ieleweke kwa wapenzi na mashabiki zangu kwamba sidaiwi chochote na mtu huyo, sina shida ya mashairi, watunzi ninao kibao pia ndani kwangu nina mashairi mengi ambayo sijayaimba hivyo sina muda ya malumbano na mtu!, wacha aendelee kuandika tu huko mitandaoni ila nasisitiza tena sina deni na mtu huyo!, kama kuna sehemu tuliandikishiana deni hilo basi anaweza kwenda katika vyombo vya sheria nami nitakwenda kujibu hoja alisema mama huyo kwa kujiamini.


Takribani wiki tatu sasa mkurugenzi wa fungakazi modern taarab Kapten temba aliandika mitandaoni na kufanya mahojiano na vituo kadhaa vya redio hapa nchini akisisitiza kwamba anamdai khadija omary kopa shilingi laki tatu kama malipo ya mashairi yake manne ambayo alimuandikia malkia huyo katika album mpya ya ogopa kopa classic bendi. Na hayo ndio majibu ya malkia huyo kwamba hadaiwi chochote na temba!. “Chanzo tamtam za pwani east africa redio”.


KHADIJA OMARY KOPA MALKIA WA MIPASHO NCHINI TANZANIA.

About the author

kidevu

Leave a Comment