Safu ya ulinzi ya Yanga inaongozwa na Lamine Moro na Bakari Mwamnyeto ambao wameokota nyavuni jumla ya mabao 11 katika mechi 21 ambazo wamecheza.
Mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar ulikusanya mabao mengi ya kufungwa ambayo ni matatu kwa kuwa awali mechi zote walizofungwa ilikuwa ni mwendo wa kufungwa bao mojamoja.
Kaze amesema:-“Wachezaji wangu sanasana wa mbele wamekuwa wakiruhusu mipira kiurahisi na kushindwa kuizuia mipira hasa tunapokuwa ndani ya uwanja.
“Makosa yetu huwa yanakuwa hasa kipindi cha kwanza, ule uwezo wa kuzuia mipira kati umekuwa ukipungua jambo ambalo limekuwa likiwaruhusu wapinzani wetu kupenya kwenye ngome yetu hivyo hilo tunalifanyia kazi na tunaamini tutakuwa imara,”.
Yanga ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi ikiwa imekusanya jumla ya pointi 49.