HABARI

KOCHA NGORONGORO HEROES ATAJA WALIPOKOSEA

 

JAMHURI Kihwelo, ‘Julio’ Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes amesema kuwa kilichosababisha timu hiyo isipate matokeo ni ugeni katika mashindano hayo.

Ngorongoro Heroes ilikuwa inashiriki michuano ya Mataifa Afrika, (Afcon) hatua ya makundi ikiwa kundi C pamoja na timu za Ghana, Gambia na Morocco. 

Katika kundi hilo Tanzania imeambulia pointi moja baada ya kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Gambia.

Ilipoteza kwa kufungwa mabao 4-0  dhidi ya Ghana na mbele ya Morroco iliambulia kichapo cha mabao 3-0.

Julio amesema:”Ugeni wa mashindano kwenye kundi letu umetufanya tushindwe kupata matokeo tofauati na wengine ambao tulikuwa nao kwenye kundi.

“Tunamshukuru Mungu tumeshiriki salama ila ushiriki wetu pia kuna kitu ambacho tumejifunza hivyo itakuwa ni safari yetu ya mafanikio kwenye mashindano mengine,”.

About the author

kidevu

Leave a Comment