HABARI

JUMA MGUNDA:KILA TUNAPOKOSEA TUNAFANYA MAREKEBISHO

 

JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Coastal Union amesema kuwa licha ya kupata matokeo yasiyoridhisha bado anapata muda wa kuongea na wachezaji wake ili aweze kuwajenga wawe bora zaidi ndani ya uwanja.

Kocha huyo ambaye anafundisha pia timu ya Taifa ya Tanzania, amekiongoza kikosi chake kwenye mechi mbili mfululizo, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na kuyeyusha pointi zote sita.

Ilikuwa mbele ya Dodoma Jiji timu yake ilipopoteza kwa kufungwa mabao 2-1  na mbele ya JKT Tanzania alipoteza kwa kufungwa mabao 2-0.

Jumla ndani ya dakika 180 amekusanya mabao manne na kufunga bao moja. Anabaki na pointi zake 23 akiwa nafasi ya 13. 

Akizungumza na Saleh Jembe, Mgunda amesema:-“Hamna namna ya kufanya ukiwa mwalimu zaidi ya kutatua yale ambayo yanakosewa ndani ya timu kikubwa ni kupata ushindi ndani ya uwanja.

“Ninatambua kwamba wapi ambapo wanakosea kisha ninawafundisha upya kwa kuwa tunapokuwa kwenye mazoezi hapo ni maandalizi ya mchezo wetu ujao na kupitia huko ninajua wachezaji wameelewa kiasi gani.

“Mechi bado zipo na ushindani ni mkubwa hivyo imani yangu ni kwamba bado tupo na tutazidi kupambana ili kupata matokeo chanya,”.

 

About the author

kidevu

Leave a Comment