HABARI

Sallam SK Afunguka Ugomvi wake na Harmonize,Tulikuwa Hatuongei Mwaka Mzima.

 


Meneja wa Diamond Platnumz ,Sallam SK kwa mara ya Kwanza amefunguka kuhusu Ugomvi wake wa muda mrefu na aliyekuwa msanii wa lebo hiyo,konde boy Harmonize.

Sallam amefunguka hayo kwenye interview yake na Salama kwenye kipindi cha Salama Na ambapo aliulizwa kwanini alikataa kumpa mkono HArmonize Hadharani Walipokutana kwenye msiba wa Agness Masogange.

Sallam amedai kuwa hakuwai kuwa na matatizo na Harmonize mpaka Pale aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam wakati huo Paul Makonda kumshtumu kuwa anavuta bangi na angempeleka central ambapo Harmonize alidai kuwa Tale ndiye aliyemchongea.Kwa upande wake Sallam anasema hakupendezwa na shtuma hizo na kununua ugomvi huo kwa kusema kuwa yeye ndiye aliyemchongea.


Sallam amedai kuwa ameishi na Harmonize akiwa WCB kwa mwaka mmoja huku Harmonize akiwa hamsalimii na ndio mana hata Harmonize alipotaka kumpa mkono hadharani eti kwa kuwa wapo kwenye msiba alikataa kwa kuwa kwake aliona kama unafiki.

About the author

kidevu

Leave a Comment