Meneja wa Diamond,Sallam Sk amefunguka kuhusu tuhuma za kuwa yeye ndiye anayembania Msanii Ali Kiba kung’ara Kimataifa.
Kwenye mahojiano yake na Salama Na Sallam amekanusha na kusema kuwa yeye asingeweza kufanya huvyo kwa sababu Ali Kiba alikuwa na meneja aitwaye Seven ambaye alikuwa na connection kila kona ya dunia.
“Kuna Wakati watu wanasema Unambania Ali Kiba wakati Ali Kiba Anafanya kazi na Seven.Seven is one of the best managers in East Africa if not Africa,sasa unambania sehemu gani?Kwa sababu mtu ana acces,Seven amefanya kazi MTV,wakati Jay z anakuja yeye ndo alikuwa anasimamia,kwa hiyo nabana sehemu gani?”,Alifunguka Sallam