HABARI

Maeneo ya kuabudu, Shule zafungwa Rwanda kukabiliana na janga la Virusi vya Corona

Abanyeshuri bo mu ishuri ryisumbuye ry'abakobwa rya Muramba, basubira mu masomo ya nijoro bari mu nzu y'uburiro (ifoto yo mu bubiko)

Serikali ya Rwanda imetangaza kuchukua hatua kadhaa za dharura kukabiliana na janga la Virusi vya Corona, saa kadhaa baada ya kutangaza kwamba raia mmoja wa India aliyewasili nchini humo Machi 8, amethibitishwa kuwa na ugonjwa huo.

Katika mahojiano na Radio Rwanda, Mawaziri Anastase Shyaka wa mambo ya ndani na Dr Ngamije Daniel wa Afya, walisema kuwa hatua hizo ni pamoja na kufungwa kwa shule zote za umma na za kibinafsi, maeneo ya kuabudu na sehemu zote za umma.
Hatua hiyo inaanza kutekelezwa kuanzia hii leo, wamesema. Bwana Shyaka alisema kwamba pia makasisi wanaelewa ukubwa wa janga hili ambalo Rwanda na dunia nzima inakabiliana nalo.
Miongoni mwa hatua hizo, Bwana Shyaka alisema kwamba matukio kama vile mikusanyiko ya watu katika maeneo ya michezo na harusini ambayo yameahirishwa na kwamba wale waliopoteza wapendwa wao watazikwa kwa namna ya kipekee.
Shirikisho la Sola la Rwanda(FERWAFA), pia limetangaza kwamba michuano yote kwa sasa itafanyika bila kuhudhuriwa na mashabiki katika viwanja vya michezo, huku shirikisho la mpira wa mkono nchini humo likiahirisha michezo yake yote.Minisitiri Anastase Shyaka yavuze ko abakuru b'amadini bumvise uburemere bw'ikibazo u Rwanda n'isi bihanganye nacyo
Waziri Anastase Shyaka amesema viongozi wa kidini wanaelewa ukubwa wa tatizo linalokumba Rwanda na dunia kwa ujumla
Waziri Shyaka pia alitoa wito kwa raia kuepuka mikusanyiko katika maeneo ya migahawani na masokoni.
Katika usafiri wa umaa, waziri Shyaka amesema kwamba hakuna abiria atakayeruhusiwa kusimama na kutoa wito kwa watu wa eneo na vikosi vya usalama kusaidia kuhakikisha hatua hizo zinatekelezwa.
Hii ni kwasababu katika maeneo ya ufasiri wa umma mfano mjini Kigali, huo na mikusanyiko mikubwa na kuhakisha kila abiria amepata kemikali ya kuosha mikono inayoua viini kabla ya kupanda kwenye usafiri, kwa mujibu wa bodi inayodhibiti usafiri.
Dr Ngamije, Waziri wa afya amesema kwamba hatua hizi kali zitasaidia katika kukabiliana na coronavirus na kutoa mfano wa maeneo mengine kama vile Hong Kong na Singapore ambako zimezaa matunda.Minisitiri Ngamije yasabye abantu kwirinda umuco wo guhana umukono mu gusuhuzanya
Waziri Ngamije ametoa wito kwa raia kuepuka tabia ya kusalimiana kwa mikono
Aidha, ofisi ya Waziri Mkuu pia imeagiza wafanyakazi wote kuruhusiwa kufanyakazi kutokea nyumbani iwapo hilo linawezekana.
Kwa misingi kwamba mgonjwa huyo aligunduliwa na virusi hivyo siku ya tano baada ya kuwasili Rwanda, Ngamije amesema:
“Huenda mtu asiwe na dalili lakini virusi hivi tayari vipo ndani ya mwili wake. Hii ndio changamoto kubwa.”
“Tuache kusalimiana kwa mikono … kwasababu hii ndiyo njia ya kwanza ya kusambaza ugonjwa huu.”
Pia aliongeza kwamba ikiwa mtu ataonesha dalili za kukohoa na mafua apige simu bila malipo kwa nambari 114, badala ya kukimblia kwenda kwenye hospitali iliyokaribu au kituo cha afya.
Wanafunzi wanaanza kurejea nyumbani
Wizara ya Elimu ya Rwanda imetangaza kwamba wanafunzi wote waanze kurejea nyumbani kuanzia wiki hii wakianzia na wale wa shule za mkoa wa kusini na mji wa Kigali.
Na Jumatatu, wanafunzi kutoka kaskazini, mashariki na magharibi pia nao wafuate mkondo kwa kurejea nyumbani.
Wizara ya Elimu imesema kwamba itagharamia usafiri wa wanafunzi.
hata hivyo, biashara zitaendelea kama kawaida nchini humo lakini watu wanahitajika kutokaribiana kwa angalau meta moja.
Afrika mashariki, kenya na Rwanda ndio nchi za hivi karibuni kutangaza kwamba zimethibitisha visa vya virusi vya corona.

About the author

kidevu

Leave a Comment