HABARI

Maalim Seif aukwaa Uenyekiti ACT – Wazalendo, Zitto Kabwe apata asilimia 73


Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe na Maalim Seif


Mshauri Mkuu wa ACT Wazalendo, Maalim Seif Sharif hamad, amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama Taifa kwa kura 337 sawa na asilimia 93.35 na kuwashinda Yeremia Maganja aliyepata kura 20 sawa na asilimia 5.55 na Shilungushela Kaheza aliyepata kura 4 sawa na asilimia 1.10.

Uchaguzi huo umefanyika usiku wa kuamkia leo Machi 15, 2020, katika mkutano mkuu wa pili wa chama hicho kwenye ukumbi wa Mlimani City.
Aidha Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama hicho, wamemchagua Zitto Kabwe kuendelea na nafasi yake ya Kiongozi Mkuu wa chama kwa kura 276 sawa na asilimia 73.6, huku mshindani wake Ismail Jussa akipata kura 92 sawa na asilimia 24.2, ambapo kura nane zimekataliwa.
Maalim Seif ambaye pia ni mshauri Mkuu anakuwa Mwenyekiti wa pili wa chama hicho cha ACT Wazalendo tangu kuanzishwa kwake mwaka 2014.
Aidha uchaguzi huo unaendeleo leo kwa ajili ya kuwapata, Makamu Mwenyekiti Bara pamoja na Makamu Mwenyekiti Zanzibar.

About the author

kidevu

Leave a Comment